Kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars Marouf Tchakei amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Oktoba 2024
Tchakei ameibuka mshindi wa tuzo hiyo mbele ya washindani wake Lusajo Mwaikenda (Azam Fc) na Pacome Zouzoua (Yanga)
Katika mwezi Oktoba Tchakei alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao akiisaidia Singida BS kushinda mechi tatu kati ya nne





