International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Novemba 09 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi Novemba 09 2024

Kocha wa klabu ya Fenerbahce Jose Mourinho, 61, bado anamipango ya kurejea katika Ligi ya Primia, na kwa sasa analenga kujiunga na klabu ya Newcastle endapo mkufunzi wake Eddie Howe, 46, ataikacha klabu hiyo yenye maskani yake katika uwanja wa St James' Park. (Guardian)

Shirikisho la Kandanda la Brazil (CBF) have limempigia simu mara kadhaa mwaka huu kocha wa Manchester City Pep Guardiola katika harakati za kumshawishi Mhispania huyo mwenye miaka 53 kuinoa timu ya taifa ya Brazil. (The Athletic)

Guardiola huenda akabadili msimamo wake wa kutopenda kufanya usajili katika dirisha la mwezi Januari ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba kikosi chake kwa kumuwania kiungo mkabaji kutoka Brazil anayekipiga katika klabu ya Atalanta Ederson, 25. (The I - subscription required)

Newcastle wanasuka mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Kameruni Bryan Mbeumo, 25, kwa dau la pauni milioni 50. (Football Insider)

Bayern Munich wanamfuatilia mshambuliaji wa klabu ya Sporting na timu ya taifa ya Sweden Viktor Gyokeres, 26, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka klabuni mwishoni mwa msimu kwa dau la wastan wa pauni milioni 60. (Sky Germany)

Arsenal inapanga kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu ili kusajili mshambuliaji mpya na si katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Independent)

Matumaini yamerejea ndani ya kikosi cha Manchester United wakati kocha mpya wa klabu hiyo Ruben Amorim akitarajiwa kuanza majukumu yake hivi karibuni. coach. (Manchester Evening News)

Kocha Hansi Flick amefanikiwa kurejesha ubora wa Barcelona kwa kuweka kanuni kali za kinidhamu, ikiwa ni Pamoja na kuwatupa benchi wachezaji wanaochelewa. (Marca - in Spanish)

Barcelona wanapanga kuwapiku Liverpool katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 22, kwa kumjumuisha wing awa Uhispania Ferran Torres, 24, kama sehemu ya uhamisho huo. (Fichajes - in Spanish)

Wachezaji wa zamani wa Arsenal Tomas Rosicky na Per Mertesacker wanajadiliwa na uongozi wa klabu hiyo wakati akitafutwa mbadala wa Edu ambaye amebwaga manyanga ya mkurugenzi wa ufundi. (Footmercato - in French)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’