International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Novemba 10 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Novemba 10 2024

Ruben Amorim anamlenga mlinzi wa Juventus Danilo, 33, kuwa usajili wake wa kwanza Manchester United katika dirisha la Januari, kwani Mbrazili huyo anamalizia kandarasi yake mwishoni mwa msimu huu. (Mirror)

Arsenal wanamfuatilia mlinzi wa Sporting Ousmane Diomande, 20, ingawa Chelsea na Bayern Munich pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (Metro)

Real Madrid wanafikiria kumsajili tena kwa dharura gwiji, Sergio Ramos, 38, huku Sevilla na beki wa zamani wa Hispania wakionekana kama mbadala wa mlinzi wa Brazil aliyejeruhiwa Eder Militao, 26. (Fichajes)

Barcelona wameondoa nia yao ya kumnunua mlinzi wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, ili kukidhi matakwa ya mshambuliaji wao chipukizi wa Hispania Lamine Yamal, 17. (Football365)

Meneja wa Barca Hansi Flick anataka kumsajili mlinzi Alphonso Davies, 24, ikiwa nahodha huyo wa Canada ataamua kutopokea ofa ya kandarasi kutoka kwa klabu ya sasa ya Bayern Munich - ingawa Real Madrid wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili na Manchester United pia wanavutiwa naye. (Christian Falk, Bild)

Liverpool wako tayari kutoa ofa ya euro 70m (£58.1m) kwa ajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush, 25. (Fichajes)

Mkataba wa kiungo wa kati wa Real Madrid Mfaransa Aurelien Tchouameni, 24, kujiunga na Liverpool pia unakaribia kuafikiwa. (Team talk)

Manchester City wanatumai kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad Martin Zubimendi, 25, ingawa Liverpool pia wanamtaka Mhispania huyo. (Football Insider)

Meneja wa zamani wa Manchester City na Italia, Roberto Mancini ndiye anayeongoza kuchukua nafasi ya Mcroatia Ivan Juric kama mkufunzi wa Roma, huku wamiliki wa klabu hiyo Marekani wakitarajiwa kuchukua hatua hiyo baada ya mechi ya Jumapili ya Serie A wakiwa nyumbani dhidi ya Bologna. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Aston Villa wanatamani sana jozi ya Real Betis ya kiungo wa kati wa Marekani Johnny Cardoso, 23, na mlinzi wa Uhispania Diego Llorente, 31 - lakini wanatarajiwa kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Tottenham Hotspur kuwania beki huyo. (Ficherio - kwa Kihispania)

Tottenham, West Ham na Chelsea zote zinafuatilia maendeleo ya beki wa Gent Archie Brown, 20, lakini mkataba wa Muingereza huyo katika klabu hiyo ya Ubelgiji hautaisha hadi 2027. (TBR Football)

Mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 21, ana "makubaliano ya kiungwana" na klabu ya sasa ya RB Leipzig kwamba ataweza kuondoka msimu wa joto ikiwa ofa itatolewa kati ya euro 70m-75m (£58m-£62m). (Philipp Hinze, Sky Sports)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’