Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

TPLB yatabiri ushindani zaidi Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Nov 2024
TPLB yatabiri ushindani zaidi Ligi Kuu

Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), imeeleza kufurahishwa kwake na ushindani mkali unaooneshwa na timu mbalimbali kwenye michezo yake inayoendelea

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almasi Kasongo, alisema kwa raundi 10 ambazo timu zimecheza Ligi Kuu imekuwa na msisimuko mkali, huku ushindani ukiongezeka tofauti na msimu uliopita

"Ligi imekuwa na ushindani mkubwa ukilinganisha na msimu uliopita, ipo kwenye raundi ya 10, timu zingine zikiwa zimecheza mechi 11, lakini unaweza ukaona kwamba timu zote walau zimepoteza mchezo mmoja, ukilinganisha na msimu uliopita katika kipindi kama hiki kulikuwa na timu ambazo bado zilikuwa hazijapoteza mchezo," alisema Kasongo

Alisema sababu nyingine inayoonesha ligi ya msimu huu imekuwa ngumu zaidi ni baadhi ya matokeo ya mechi kuamuliwa dakika za mwisho

"Vile vile unaweza kuona ni jinsi gani michezo ilivyokuwa na ushindani mkubwa, tumeona michezo mingi ikiamuliwa dakika za jioni, dakika za nyongeza, kwenye sekunde za mwisho kabisa, hii inadhihirisha ushindani mkubwa," alisema Ofisa Mtendaji Mkuu huyo

Alisema hiki ndicho mashabiki wengi wa soka nchini na Watanzania walikuwa wakihitaji, kupata ligi ambayo ni ngumu, yenye ushindani, ambayo haitabiriki, huku akitabiri kuwa kadri inavyozidi kusonga mbele, ndivyo itakavyokuwa na ushindani zaidi kuliko huu uliopo sasa

"Itoshe kusema kile ambacho Watanzania walikuwa wanakitarajia kupata ligi yenye ushindani sasa hivi kinaonekana, matarajio yetu ni kwamba hadi itakapofika Aprili na Mei ushindani utazidi kuwa mkali zaidi kuliko huu kwa sababu ni kipindi baadhi ya timu zitakuwa zinaelekea kwenye ubingwa, zingine kuwania nne bora kwa ajili ya kucheza mechi za kimataifa, kuna zitakazokuwa zinapambana kutocheza 'play off', na zipo ambazo zitakuwa zinapigana kutoshuka daraja," alisema

Mpaka wakati ligi hiyo imesimama kupisha Kalenda ya FIFA, Simba inaongoza ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 25, Yanga iko nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, Singida Black Stars ni ya tatu na pointi zake 23, huku Azam FC ikikamata nafasi ya nne, pointi zake 21

IPP Media

More Stories

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
2h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
4h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
8h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
9h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
9h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
22h ago
READ MORE β†’
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
1d ago
READ MORE β†’