Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, KMC

TPLB kupitia maombi ya Yanga kuhamia KMC Complex

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Nov 2024
TPLB kupitia maombi ya Yanga kuhamia KMC Complex

Bodi ya Ligi imesema imepokea barua ya klabu ya Yanga inayoomba kuhama kutoka, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na kuhamia, KMC Complex kwa sasa wapo kwenye mchakato na kutazama sababu pamoja na kanuni ili kutoa uamuzi

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almasi Kasongo, alisema kuwa barua hiyo ilipokelewa juzi na sasa iko kwenye mchakato na siku si nyingi watatoa maamuzi ya kuwakubalia ama vinginevyo

Klabu ya Yanga juzi ilitangaza kuhama Uwanja wa Azam Complex na kuhamia KMC Complex, katika michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la FA ambalo bado halijaanza

"Tumepokea barua ya Yanga kutaka kucheza Uwanja wa KMC Complex, nadhani leo (Jumatatu) siku ya kazi, vijana wataanza kazi ya kuichakata, baada ya hapo tutakuwa na nafasi nzuri na kutangaza maamuzi ya Bodi"

"Barua inaeleza makusudio yao ya kuhama kutoka Uwanja wa azam Complex kwenda KMC Complex, Mwenge, wameeleza sababu zao lakini zinabaki kuwa siri yetu baina ya klabu na Bodi na wamiliki wa uwanja wa Azam"

"Sababu zinafikirisha, zina mashiko au hazina mashiko, hayo yote yapo kwenye mchakato, sisi tunautazama mpira zaidi, Bodi ni chombo cha klabu zote kwa hiyo kipo kwa maslahi yao kama chombo chao, tunakaa kujiridhisha," alisema

Hata hivyo alisema yote hayo ni lazima yawe kwenye kanuni, hivyo pia watakaza kanuni zinasemaje, lakini bila kuacha maslahi ya kimpira

Baada ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Tabora United Alhamisi iliyopita kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache tu tangu kupokea kipigo kingine cha bao 1-0 dhidi ya Azam FC, tetesi zilianza kusikika kuwa viongozi walikuwa na mpango wa kutaka kuhama kwenye uwanja huo

Juzi klabu hiyo ilitoa taarifa yake rasmi kupitia Ofisi ya Mtendaji Mkuu kuwa timu hiyo ikielezea kuhamia Uwanja wa KMC

Hata hivyo uwanja huo kwa sasa unatumiwa na timu ya Simba na KMC kama viwanja vya nyumbani hivyo kama Yanga itakubaliwa, basi ni wazi kuwa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara itabadilika, hasa tarehe ambazo timu hizo zilitakiwa kucheza kwa siku moja kwenye viwanja vya nyumbani

IPP Media

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’