International,Transfer News,Barcelona, PSG, Inter

Messi kumalizia soka Argentina

Joel JJ By Joel JJ
12 Nov 2024
Messi kumalizia soka Argentina

Kwa mujibu wa mtandao wa GOAL, Lionel Messi anataka kujiunga na timu yake ya utotoni, Newell's Old Boys, baada ya kumalizika kwa msimu wa MLS wa mwaka 2025

Inaelezwa Messi ambaye ameshindwa kuisaidia timu yake kwenda hatua ya nusu fainali ya mtoano wa ligi Ukanda Mashariki licha ya kufunga mabao 20 katika msimu wa kawaida, anachosubiria kwa sasa ni kumalizika kwa makataba wake mwisho wa msimu huu.

Kocha wa Miami, Tata Martino ameonyesha wasiwasi wa kuwa staa huyo anaweza kuondoka ingawa alishindwa kuweka wazi ni lini.

"Kwa kweli sijui ni muda gani Messi anaweza kuendelea kuwa hapa, ni kweli muda wa mkataba wake unakaribia kuisha lakini siwezi kusema yupo hapa kwa muda mfupi," alisema Martino alipokuwa akizungumzia hatma ya Messi kikosini hapo

Miami ambayo imeshindwa kufuzu kwenda hatua ya mtoano kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Marekani tayari imeshachaguliwa kuwa timu itakayoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2025 itakayofanyika huko Marekani jambo lililozua malalamiko kwa timu nyingi pinzani za Marekani.

FIFA iliitangaza Miami kuwa itashiriki Kombe la Dunia kwa kigezo cha kushinda tuzo ya Supporter Shield inayotolewa na waandaaji wa Ligi Kuu ya Marekani kwa timu iliyofanya vizuri katika msimu wa kawaida na wao watakuwa ndio wenyeji

Messi na timu yake wamefanya vibaya msimu huu baada ya kutolewa katika raundi ya kwanza ya mtoano na Atalanta United.

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
55m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →