International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Novemba 13 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Novemba 13 2024

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anafikiria kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, na mlinzi mwenzake Mholanzi Sepp van den Berg, 22, ambaye alijiunga na Brentford kutoka Liverpool msimu uliopita. (Football Transfers )

Wakala wa mshambuliaji wa Canada Jonathan David amewaambia wanaomtaka kama vile Juventus, Inter Milan, Liverpool na Manchester United kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anataka kandarasi yenye thamani ya £5m kwa mwaka ili kujiunga nao kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake na Lille utakapokamilika msimu ujao (Tuttosport - In Itali)

Juventus wanataka kumchukua mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, kwa mkopo kutoka Manchester United mwezi Januari. (Tuttosport - In Itali)

Arsenal na Liverpool ni miongoni mwa klabu kuu za Ulaya zinazotaka kumuongeza kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt na Uswidi Hugo Larsson, 20, kwenye klikosi chao mwezi Januari. (Team Talks)

Chelsea ni miongoni mwa klabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Newcastle na Crystal Palace, ambao wanamtaka beki wa kati wa Benfica Mreno Tomas Araujo, 20. (O Jogo - In Portuguese)

Manchester United imekuwa ikitafuta chaguo la kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Alvaro Carreras, 21, ambaye walimuuza kwa Benfica msimu wa joto. (Marca - In Spanish)

Liverpool wamevutiwa na Daniel Svensson wa Sweden, huku Manchester United na Arsenal FC pia wakiwa miongoni mwa klabu zinazomuwania Nordsjælland beki wa kushoto, 22. (Teamtalk)

Barcelona wamemuorodhesha mshambuliaji wa Porto Mhispania Samu Omorodion, 20, kama mbadala wa Robert Lewandowski wa Poland, 36. (El Nacional - In Spanish)

Real Madrid wamemuweka beki wa kati wa Al-Nassr wa Uhispania Aymeric Laporte, 30, na beki wa kulia wa Tottenham Pedro Porro, 25, kwenye rada yao. (Relevo - In Spanish)

Mkurugenzi wa ufundi David Weir na msaidizi wake Mike Cave wameongoza marekebisho ya idara ya uajiri ya Brighton na kuhusisha kuondoka kwa maskauti kadhaa, licha ya klabu hiyo kufanikiwa katika misimu ya hivi majuzi. (Telegraph - Subcription Required)

Mshambulizi wa zamani wa Roma Vincenzo Montella ndiye anayeongoza kuwania nafasi ya kocha mpya wa Giallorossi na anaonekana kuwa tayari kuvunja mkataba wake kama kocha wa Uturuki, ingawa itamgharimu karibu pauni milioni moja kufanya hivyo. (Gazzetta dello Sport - In Itali)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’