Klabu ya Fountain Gate imethibitisha kumsajili mshambuliaji Yusuph Athumani akisaini mkataba wa miaka miwili
Yusuph ametua Fountain Gate akiwa mchezaji huru mkataba wake na Yanga ukimalizika mwishoni mwa msimu uliopita
Msimu uliopita Yanga ilimtoa kwa mkopo Yusuph kuitumikia Coastal Union kabla ya kutimkia West Almeria ikiwa ni mkopo pia




