Waamuzi wanne wa Tanzania wako Afrika Kusini kwa ajili ya kuchezesha mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baina ya Lesotho dhidi ya Afrika ya Kati
Mechi hiyo itachezwa leo kuanzia saa 10:00 jioni kwa muda wa Afrika Mashariki
Refa wa kati atakuwa ni Ahmed Arajiga akisaidiwa na Frank Komba na Hamdani Said huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Sasii
Lesotho inashika mkia katika kundi B la mashindano hayo ikiwa na pointi moja, Morocco inaongoza ikiwa na pointi 12 huku Gabon ikikusanya pointi saba na Afrika ya Kati ina pointi tatu