Local,Normal News,Yanga, Azam, Singida, Coastal

Azam Fc, Gamondi wakumbana na rungu la TPLB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Nov 2024
Azam Fc, Gamondi wakumbana na rungu la TPLB

Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi, imeitoza klabu ya Azam Fc faini ya Sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa kola la kuzuia wapigapicha wa mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga, Azam TV kurekodi picha jongeo wakati timu hiyo ikiingia katika uwanja wa Azam Complex, kuelekea mchezo dhidi ya Yanga

Kulingana na taarifa ya Kamati, kitendo hicho ni uvunjifu wa masharti ya udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, jambo ambalo ni kinyume na kanuni

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 16:1(1.7) ya Ligi Kuu kuhusu Udhamini

Kamati hiyo pia imemfungia mechi tatu aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kumsukuma na kumuangusha chini kocha wa viungo wa klabu ya Singida Black Stars, Sliman Marloene, baada ya mabishano yaliyotokea wakati timu hizo zikienda mapumziko katika mchezo dhidi ya Singida BS kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha

Kamati pia imefuta adhabu ya kadi ya manjano aliyoonyeshwa mchezaji Ibrahim Abdullah wa klabu ya Yanga katika mchezo dhidi ya Coastal Union, baada ya kujiridhisha kupitia picha jongeo na taarifa za wataalam kuwa mchezaji huyo hakustahili adhabu hiyo

Uamuzi huo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 12:8 ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi

Klabu ya Singida Black Stars imetozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuingilia mazoezi ya klabu ya Yanga siku moja kabla ya terehe ya mchezo baina ya timu hizo

Timu ya Singida iliingia kwenye uwanja wa New Amaan Complex katika muda wa kikanuni wa klabu ya Yanga kufanya mazoezi, jambo ambalo lilivuruga programu ya mazoezi hayo ya Yanga ambalo yalikuwa yakiendelea, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:45 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’