Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inatupa karata muhimu katika michuano ya kuwania kufuzu Afcon 2025 kwa kumenyana na Ehiopia katika mchezo utakaopigwa Kinshasa, DR Congo saa 1 usiku
Matumaini ya Tanzania kufuzu kwa michuano hiyo yameshikiliwa na mechi mbili za kuhitimisha kampeni ya kuwania kufuzu dhidi ya Ethiopia na Guinea
Tanzania inahitaji kushinda leo ili kujiweka katika mazingira mazuri kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya Guinea ambao utapigwa Novemba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika msimamo wa kundi H Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama nne nyuma ya Guinea inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama sita
DR Congo ambao ni vinara wa kundi tayari wamefuzu wakiwa na alama 12 wakat Ethiopia yenye alama moja inaburuza mkia
Vijana wa Kaimu Kocha Mkuu Hemed Morocco hawahitaji matokeo ya aina nyingine zaidi ya ushindi huku DR Congo ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu
Kila la kheri Stars....



