International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Novemba 18 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Novemba 18 2024

Manchester United wameambiwa kuwa Sporting huenda hawana budi ila kumuuza mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, lakini sio katika dirisha la uhamisho la Januari. (Mirror)

Manchester United wanajaribu kupata mkataba wa kumnunua winga wa Sporting mwenye umri wa miaka 17 Mreno Geovany Quenda. (A Bola - kwa Kireno)

Barcelona wanafikiria kumpa kipa Wojciech Szczesny, 34, mkataba mpya wiki chache baada ya raia huyo wa Poland kujiunga na klabu hiyo. (Marca kwa Kihispania)

Mkufunzi wa Aston Villa Unai Emery anaweza kuamua kumuuza mlinzi wa Brazil Diego Carlos mwenye umri wa miaka 31 mwezi Januari. (Football Insider)

Winga wa Brazil Neymar anatazamiwa kurejea Santos huku klabu yake ya Saudi Arabia Al-Hilal ikifadhaishwa na matatizo ya jeraha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Cesar Luis Merlo)

Kiungo wa kati wa Benfica na Uturuki Orkun Kokcu, 23, amesifu athari ambayo meneja wa Liverpool Arne Slot amekuwa nayo kwenye maisha yake ya soka huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia Anfield. (Liverpool Echo)

Fulham wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Igor Jesus, 23, kutoka Botafogo . (TBR Football)

Tottenham Hotspur wanaangalia uwezekano wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Harry Winks, 28, baada ya kumuuza kwa Leicester mwaka jana. (Fichajes - kwa Kihispania) Arsenal bado wanafuatilia hali ya mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 katika klabu ya Juventus . (Rudy Galetti)

Crystal Palace wana nia ya kusajili mshambuliaji wakati wa uhamisho wa Januari lakini wana bajeti ndogo tu. (NipeSport) Mshambuliaji wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, anaweza kuondoka Napoli kwa vile mazungumzo yake ya kandarasi yamekwama huku Barcelona na Paris St-Germain wakimtaka . (Goal)

Hakuna mpango wa Paul Pogba kufanya mazoezi katika klabu ya Manchester United baada ya kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 kuondoka Juventus . (Talksport)

Frank Lampard anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea watano ambao Coventry City watazungumza nao kuhusu kibarua chao cha meneja kilicho wazi. (Telegraph - usajili unahitajika)

West Ham na Southampton zote zinawawinda mapacha Cole na Dylan Williams wenye umri wa miaka 16 huku kiungo hao wa Uskoti kwa sasa wakiwa Airdrie . (Sun)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’