Local,Transfer News,Simba

Fadlu matumaini kibao kwa Mpanzu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Nov 2024
Fadlu matumaini kibao kwa Mpanzu

Wakati dirisha dogo la usajili likikaribia kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewaambia wanachama na mashabiki wa Simba kuwa, wakae tayari kumuona mchezaji mpya, Elie Mpanzu, akisema ataongeza kitu ndani ya kikosi chake kutokana na kipaji kikubwa alichonacho, huku akimtabiria makubwa

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini, alisema jana kuwa anaamini kutokana na kipaji alichonacho, atafunga mabao mengi na kuwasaidia wenzake kuwapa pasi za mwisho kwa ajili ya kupambania nembo ya klabu hiyo

Ijumaa iliyopita, mchezaji huyo alicheza kwa dakika kadhaa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam na kutoka sare ya bao 1-1, lakini haikuhudhuriwa na mashabiki

"Tunategemea kuwa atafunga sana na atatengeneza nafasi nyingi kwa wenzake, tunategemea atafiti kwenye kila mfumo wetu, tunamtegemea sana Mpanzu kuleta upinzani ndani ya kikosi," alisema kocha huyo

Mpanzu ataanza kuitumikia Simba kwenye mashindano rasmi Desemba 15 wakati timu hiyo itakapocheza mechi yake ya raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, utakaopigwa, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku akitarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu itapovaana na KenGold, Desemba 18, Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam

"Mpanzu ni mchezaji wa kipekee sana, tumekaa naye vikao vingi kuona ni sehemu gani anaweza kuzoea na kuwa huru akicheza uwanjani, tunataka azoee mipango yetu ajue nini cha kufanya akiwa na mpira, nafasi ipi achukue uwanjani akiwa na mpira na hata asipokuwa nao"

"Tumekaa naye vikao kuangalia ni namna gani anaweza kushambulia kulingana na wapinzani wetu wanavyocheza, nini tunafanya tunapokuwa tuna mpira, muda ambao hatuna, kinachobaki ni yeye mwenyewe kujiweka sawa na kuzoea mifumo yetu kwa kuwa bado hajaanza kucheza michezo ya mashindano, ila hii michezo ya kirafiki itamsaidia," alisema

kocha huyo. Mabosi wa Simba walimpa mkataba winga huyo raia wa Jamhuri ya Kidemkorasi ya Congo, kabla ya dirisha dogo la usajili

Awali, Mpanzu, alikuwa asajiliwe na Simba kipindi cha dirisha kubwa, lakini dili liliharibika baada ya kutimkia nchini Ubelgiji kwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Genk, ambayo hayakufanikiwa

Baada ya kutofanikiwa na kumaliza mkataba wake na AS Vita, Simba ilirejea kwenye meza ya mazungumzo na mchezaji huyo, ikampa mkataba haraka kabla ya dirisha dogo ili kuepuka dili hilo kuvunjika tena

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’