Local,Normal News,Yanga, Hilal

Al Hilal yaiwahi Yanga Dar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Nov 2024
Al Hilal yaiwahi Yanga Dar

Kikosi cha Al Hilal, leo Jumanne Novemba 19, 2024 kimeanza safari kutoka Libya kuja Tanzania kwaajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Novemba 26 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Wakati kikosi hicho kikianza safari hiyo, kocha mkuu wa timu hiyo, Florent Ibenge amesema ana siku nne pekee za kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga.

Ibenge amebainisha kwamba, siku hizo nne zimekuja kutokana na kwamba hivi sasa ana wachezaji 13 pekee huku kundi kubwa likiwa na majukumu katika timu zao za taifa kucheza mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025

"Siwezi kusema nimekiandaa kikosi kwaajili ya mechi hiyo (dhidi ya Yanga) kwani huku Libya nilikuwa na wachezaji 13 tu wengine wakiwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa"

"Naweza kusema nina siku nne tu za kukiandaa kikosi changu kikiwa na wachezaji wote," alisema Ibenge.

Katika safari yao ya kuja Tanzania, Al Hilal ilitoka Mauritania na kuweka kambi ya siku nane nchini Libya na kucheza mechi mbili za kirafiki, moja ikishinda 2-0, nyingine ikitoka suluhu dhidi ya Al Ittihad.

Kutokana na nchini Sudan ligi kusimama kwa muda mrefu kutokana na hali ya kiusalama kutokuwa sawa, Al Hilal kwa sasa inashiriki Ligi Kuu nchini Mauritania ambapo imecheza mechi saba na kushinda tano huku ikipata sare mbili, inaongoza msimamo wa Ligi hiyo kwa pointi 17.

Yanga na Al Hilal zitakututana katika mchezo huo wa kwanza Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati Al Hilal ikiwa safarini, jana kocha mpya wa Yanga, Sead Ramovic na msaidizi wake, Mustafa Kodro walianza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho baada ya kuchukua mikoba ya Miguel Gamondi aliyeondoshwa Novemba 15 mwaka huu sambamba na msaidizi wake Moussa N'Daw

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’