Local,Normal News,Prisons, JKT

Prisons yajipanga na Derby ya majeshi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Nov 2024
Prisons yajipanga na Derby ya majeshi

Nahodha wa Prisons, Jumanne El Fadhili, amekiri kuwa mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, utakuwa mgumu kwani haijawahi kuwa mechi rahisi zinapocheza timu za majeshi hasa timu hizo mbili

Akizungumza juzi kuelekea kwenye mchezo huo, El Fadhili alisema katika mchezo huo timu yoyote itakayojipanga vizuri inaweza kuibuka na ushindi huku akiongeza kuwa wao Prisons wapo kwenye maandalizi kabambe kwa ajili ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi

"Hizi ni timu za majeshi na zinajuana, mechi huwa ni ngumu sana, inakuwa na matumizi ya akili na nguvu kwa wakati mmoja, hakuna mchezo wowote rahisi kati yetu na wao (JKT), lakini atakayejipanga vizuri atashinda"

"Sisi tutakuwa ugenini wao nyumbani, tunakwenda kwa tahadhari sana, pamoja na hayo hilo halizuii sisi kupambana na kupata matokeo ya ushindi kama tutajipanga vizuri," alisema nahodha huyo

Naye golikipa wa timu hiyo, Edward Mwakyusa ambaye kwa sasa ameanza kuaminiwa na kuwekwa langoni badala ya Mussa Mbisa, amesema amejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika dabi hiyo ya timu za majeshi

"Nashukuru kocha ameanza kuniweka langoni, ameanza kuniamini na alikuwa ananiambia we tulia ipo siku utacheza, na kweli, nimeanza kucheza na bahati nzuri nimefanya vizuri sijawaangusha wenzangu na naahidi sitawaangusha katika michezo yote ambayo nitakaa langoni," alisema

Kipa huyo ameanza kupewa nafasi ya kuanza badala ya kipa namba moja, Mbisa ambaye Kocha Mkuu, Mbwana Makata alikaririwa akisema amekuwa akifanya makosa mengi na kusababisha timu kufungwa mabao mepesi

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Prisons inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 10, ikishinda miwili, sare nne na kupoteza michezo minne

IPP Media

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
58m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’