Tanzania imefanikiwa kufuzu kwa fainali za Afcon 2025 kwa mara ya nne baada ya kuichapa Guinea bao 1-0 katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Alikuwa ni Saimon Msuva aliyefunga bao pekee la Stars katika dakika ya 61 akimalizia kwa kichwa krosi ya Mudathir Yahya
Kwa mara nyingine Tanzania inakwenda kuandika historia kwa kufuzu Afcon katika ardhi ya nyumbani baada ya kufanya hivyo mwaka 2019 dhidi ya Uganda
Hii ni mara ya kwanza kwa makocha wazawa chini ya Hemed Morocco kuipeleka Tanzania katika michuano ya Afcon 2025
Tanzania inamaliza nafasi ya pili kundi H ikifikisha alama 10 huku Guinea wakisalia nafasi ya tatu wakiwa na alama 9
Ni shangwe na vifijo kwa Watanzania baada ya kuishuhudia timu yao ikifuzu fainali za Afcon kwa mara nyingine