Wapinzani wa Yanga katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika, Al Hilal wamewasili nchini leo kuelekea mechi ya kwanza ya makundi CAF CL
Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Hilal katika mchezo wa kwanza kundi A ambao utapigwa Jumanne ijayo, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Dar, Kocha Mkuu wa Al Hilal, Florent Ibenge, amesema wamekuja mapema Dar ili kuzoea hali ya hewa na pia kupata muda wa maandalizi ya mchezo huo
Ibenge amebainisha kuwa kikosi chake kiliwakosa nyota wengi ambao walikuwa katika majukumu ya timu za Taifa, hivyo watatumia siku zilizobaki kufanya mazoezi ya pamoja kabla ya mchezo dhidi ya Yanga