Local,Normal News,Simba, Pamba

Simba safarini Mwanza kuifuata Pamba Jiji leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Nov 2024
Simba safarini Mwanza kuifuata Pamba Jiji leo

Usiku wa leo vinara wa ligi kuu ya NBC, Simba wataondoka jijini Dar es salaam kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji. Mchezo huo utapigwa Ijumaa, Novemba 22 katika uwanja wa CCM Kirumba

AKizungumza na wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali alisema msafara wa Simba utakaoondoka utajumuisha wachezaji ambao walikuwa katika majukumu ya timu za Taifa

Ahmed alithibitisha wachezaji Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Aishi Manula, Kibu Denis na Moussa Camara watakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachosafiri huku mshambuliaji Steven Mukwala aliyekuwa na timu ya Taifa ya Uganda akitarajiwa kuungana na Simba jijini Mwanza mapema Alhamisi

Aidha kiungo Yusuph Kagoma na winga Joshua Mutale hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachosafiri wakiwa ni majeruhi

Simba inakwenda Mwanza ikiwa ndio vinara wa ligi kuu wakikusanya alama 25 baada ya mechi 10 alama moja mbele ya watani zao Yanga wanaoshika nafasi ya pili

Simba inatarajiwa kutumia mchezo dhidi ya Pamba kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho hatua ya makundi dhidi ya Bravos utakaopigwa Jumatano, Novemba 27 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
43m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’