International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Novemba 21 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Novemba 21 2024

Liverpool na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25. (Sun)

Manchester City wapo katika nafasi nzuri ya kumpata kiungo wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 21, huku Real Madrid na Liverpool zikimkosa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Caught Offside)

Beki wa klabu ya Santos Joao Victor de Souza, 18, ananyatiwa na Chelsea lakini klabu hiyo ya Ligi ya Premia itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona kumnunua Mbrazil huyo. (AS - kwa Kihispania)

Beki wa Sporting na Ivory Coast Ousmane Diomande, 20, amezungumza na Ruben Amorim wa Manchester United kuhusu kuungana tena na kocha wake wa zamani Old Trafford. (Metro)

Ajenti Jorge Mendes anajaribu kupata uhamisho wa winga wa Sporting wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ureno Geovany Quenda, 17, huku akitarajiwa kutua Manchester United. (Team Talk)

Kiungo wa kati wa Rosenborg na Norway Sverre Nypan, 17, hatajiunga na Manchester United hadi atakapohakikishiwa kuhusu soka la kikosi cha kwanza. (Give Me Sport)

Aliyekuwa mkufunzi wa muda wa Manchester United Ruud van Nistelrooy ana nia ya kusalia kwenye Ligi ya Premia huku kukiwa na nafasi za ukocha katika klabu za Southampton, Wolves na Crystal Palace. (Football Insider)

West Ham wako tayari kumuuza mchezaji aliyesajiliwa katika majira ya kiangazi Guido Rodriguez, 30, mwezi Januari, na kurejea katika klabu ya zamani ya Real Betis kumsaka kiungo huyo wa Argentina. (Estadio Deportivo - kwa Kihispania)

Southampton, Brighton na Ipswich wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Vasco de Gama raia wa Brazil Rayan, 18, mwezi Januari. (Give Me Sport)

Nottingham Forest itahitaji zaidi ya pauni milioni 70 kumnunua beki wa Brazil Murillo, ambaye anawindwa na Liverpool. (Football Insider)

Manchester City wako tayari kumenyana na Paris St-Germain na Juventus kumnunua kiungo wa kati wa Atalanta na Brazil Ederson, 25. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Besiktas wanatumai kumsajili kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, bila malipo kandarasi yake na Arsenal itakapokamilika msimu huu. (Sabah - kwa Kituruki)

West Ham, Brighton na Fulham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uingereza Josh Brownhill, 28, ambaye bado hajasaini mkataba mpya na Burnley. (TBR)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’