Local,Normal News,Tabora, Singida

Tabora United imepania kuendeleza ubabe NBC PL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Nov 2024
Tabora United imepania kuendeleza ubabe NBC PL

Baada ya kufanya sherehe ya wiki nzima kwa kuifunga Yanga mabao 3-1 Novemba 7, mwaka huu, sasa kikosi cha Tabora United kimeanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars huku kikitamba kuwa timu hiyo itakipata kile ambacho kiliwakuta wenzao katika mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Jumapili ijayo

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Christina Mwagala, amesema wachezaji wote wa timu hiyo walianza mazoezi juzi, isipokuwa Salum Chuku ambaye ni majeruhi na wamekuwa na ari na nguvu kubwa baada ya kuonekana kuwa mashujaa kwa kuifunga Yanga

"Baada ya kupata heshima kubwa na zawadi kutoka kwa watu mbalimbali na mashabiki wa soka nchini, wachezaji wa Tabora United wameanza mazoezi kwa ari na nguvu kubwa, tunachohitaji kwa sasa ni kuendeleza mlolongo wa ushindi, hatukuanza vizuri ligi, lakini tumeshinda mechi tatu mfululizo, tunataka tuendeleze ushindi na lengo letu mwisho wa msimu tuwe ndani ya zile timu nne za juu, ndiyo tunalohitaji msimu huu," alisema Mwagala

Aliitahadharisha Singida Black Stars kuwa kama wakija vibaya, basi kile ambacho kiliwakuta Yanga nao kitawakuta na huenda idadi ya mabao ikawa kubwa zaidi

"Hapa tunaandaa dozi kwa Singida Black Stars, tunawaambia wakija ovyo, watakutana na alichokutana nacho Yanga, na yeye vile vile kitakwenda kumkuta, kwa sababu mchezo huu unachezwa nyumbani na mashabiki wetu wengi watahudhuria kwani wamehamasika sana baada ya ushindi dhidi ya Yanga, kutokana na hilo hatutaki kuwapa tena huzuni na kuwapoteza mashabiki wetu," alisema Ofisa Habari huyo

Baada ya kutofanya vizuri kwenye michezo kadhaa ya Ligi Kuu kiasi cha kumfukuza kocha wake, Francis Kimanzi, hasa baada ya kuchapwa mabao 4-2 dhidi ya JKT Tanzania, Oktoba 18, mwaka huu, timu hiyo ilishinda mechi tatu mfululizo, ikiifunga Pamba Jiji bao 1-0, Mashujaa FC 1-0, kabla ya kuitwanga Yanga mabao 3-1

Ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 17, ikicheza mechi 11, ikishinda tano, sare mbili na kupoteza nne.

More Stories

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
3h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
5h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
9h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
9h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
10h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
22h ago
READ MORE β†’
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
1d ago
READ MORE β†’