Simba ameunguruma uwanja wa CCM Kirumba akiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi wakipeleka mashambulizi mfululizo katika lango la Pamba Jiji
Mashambulizi hayo yalizaa matunda dakika ya 23 baada ya Lionel Ateba kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati
Alikuwa Ateba aliyeutumbukiza mpira kimiani na kuiandikia Simba bao muhimu ambalo limewahakikishia alama tatu katika mchezo mgumu uliotawaliwa na matumizi ya nguvu
Kipindi cha kipi Pamba Jiji walizinduka lakini haikuwa rahisi kwao kuipenya ngome ya Simba iliyokuwa chini ya mabeki Che Malone Fondoh na Carabou Chamou huku mlinda lango Moussa Camara akifanya kazi ya ziada kuikoa michomo ya washambuliaji wa Pamba Jiji
Ni ushindi ambao unaifanya Simba izidi kujiimarisha kileleni katika msimamo wakifikisha alama 28