International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Novemba 24 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Novemba 24 2024

Meneja mpya wa Manchester United Ruben Amorim ameweka kipaumbele cha kumsajili mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres kutoka klabu ya zamani ya Sporting msimu ujao lakini Manchester City pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Sunday Mirror)

Manchester United imefanya mawasiliano na Real Madrid kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo Eduardo Camavinga, 22, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa hana nia ya kutaka kuondoka. (Bernabeu Digital – In Spanish)

Klabu hiyo ya Old Trafford pia inamfuatilia mlinzi wa pembeni wa Paris St-Germain Mreno Nuno Mendes, 22, ambaye alicheza chini ya Amorim huko Sporting. (Mail on Sunday)

Lakini mabeki watatu walioteuliwa na wamiliki wa Manchester United Ineos ni mchezaji wa kimataifa wa Canada na Bayern Munich Alphonso Davies, 24, Mserbia Milos Kerkez, 21 kutoka Bournemouth na mlinzi wa Benfica Mhispania Alvaro Fernandez Carreras, 21 - ambaye aliondoka Old Trafford msimu uliopita wa joto. (Express)

Aston Villa wamejiunga na klabu kadhaa za Italia kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, kwa mkopo mwezi Januari. (Caught Offside) Arsenal wanaweza kutoa ada ya kubwa kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, msimu ujao. (Fichajes – In Spanish)

Manchester City wanajitayarisha kumtafuta kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 20. (Teamtalk)

Everton wanataka kumsajili winga wa Botafogo na Brazil Luiz Henrique, 23, huku meneja Sean Dyche akijaribu kuboresha safu yake ya ushambuliaji. (Football Insider), Tottenham na Liverpool wameungana na Barcelona katika mbio za kumsajili beki wa pembeni wa Uholanzi Devyne Rensch, 21, kutoka Ajax. (Diario Sport – In Spanish)

Chelsea wamesalia kuwa mashabiki wakubwa wa mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, lakini Seagulls watadai pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo. (TeamTalks)

Manchester City wanaweza kukatiza mipango ya Chelsea ya kumsajili mshambuliaji wa Ipswich Town Liam Delap, 21, kwa kuwa wana kipengele cha kumnunua tena kwa pauni milioni 20 mchezaji waliyemuuza tu msimu wa joto. (Express)

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 Lee Carsley ana furaha kukataa nafasi ya usimamizi wa klabu hiyo kwa matumaini ya kurithi mikoba ya Thomas Tuchel kama meneja wa Uingereza mwaka wa 2026. (The Sun)

Beki wa zamani wa Uswidi na Aston Villa Olof Mellberg anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya St Louis City. (Goal)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’