Local,Normal News,Yanga, Hilal

Kocha Yanga aipania Al Hilal

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Nov 2024
Kocha Yanga aipania Al Hilal

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema katika kikosi chake kila mchezaji atakuwa na mchango wake kwani timu yake haina mchezaji staa

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga ambayo ni mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal, Ramovic amesema pamoja na kuwa ni mara yake ya kwanza kuongoza timu katika michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa, anajivunia kukiongoza kikosi chenye wachezaji bora wenye vipaji

Ramovic amesema anaamini mafanikio katika kazi yake yatatokana na mchango wa kila mchezaji na hivyo atahitaji kuona kila mmoja anajituma ili kuhakikisha wanafikia malengo

Ramovic amesema licha ya ubora wa kikosi chake lakini wanakwenda kucheza dhidi ya timu bora pia katika michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa hivyo atahitaji wachezaji kuwa na nidhamu katika mchezo huo pamoja na kujituma

"Yanga ni timu bora sana, lakini tunakwenda kucheza na timu bora pia hivyo tunahitajika tuwe makini sana. Tunapaswa kuwa na utayari kiakili na kisaikolojia kwani tunakwenda kwenye mechi ngumu sana. Hata hivyo ninayo furaha kubwa sana kuiongoza Klabu kubwa kwenye mashindano makubwa"

"Hii ni mara yangu ya kwanza kwenye ligi ya mabingwa. Ni jambo la kheri sana kwangu kushiriki mashindano haya makubwa nikiwa na timu kubwa ya Yanga. Falsafa yangu kubwa ni nidhamu na kujituma. Napenda kuona wachezaji wakicheza kama timu, haijalishi unatumia mfumo gani kama wachezaji wako hawana umoja ni ngumu kupata matokeo"

"Kwenye timu yangu sina mchezaji mashuhuri staa kuliko mwingine. Wachezaji wote nawapa haki sawa kwa kuzingatia juhudi zao kwenye uwanja wa mazoezi. Ili tushinde lazima wachezaji wawe na umoja. Natambua ubora wa kila mchezaji lakini jambo la muhimu kwangu ni namna gani mchezaji anatumia uwezo wake kuipa timu matokeo," alisema Ramovic

Ramovic amewataka mashabiki kujitokezakwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuwa sehemu ya mafanikio ya timu yao katika mchezo dhidi ya Al Hilal

"Mashabiki ni sehemu ya timu yangu na mara zote nimekuwa rafiki yao, bahati kwangu nimekuja kwenye Klabu yenye mashabiki bora Afrika, naamini kesho watakuja kwa wingi uwanjani kunikaribisha na kuisapoti timu ili tupate matokeo mazuri"

"Mashabiki wananiita 'German Machine', lakini mimi ukiniuliza ningependa kuitwa Tanzanian Machine, nataka kufurahi pamoja na watu wa hapa na kuhakikisha klabu hii inapata mafanikio," alisema Ramovic

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
29m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’