Local,Normal News,Simba, Bravos

Fadlu aweka mkakati wa ushindi dhidi ya Bravos Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Nov 2024
Fadlu aweka mkakati wa ushindi dhidi ya Bravos Fc

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kwanza hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Bravos Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Fadlu amesema wamekuwa wakijiandaa na mchezo huu tangu wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA, leo watakamilisha maandalizi tayari kwa mchezo huo

"Niseme sisi tupo tayari kwa mchezo huu. Tulianza maandalizi ya mechi hii wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA. Tuko hatua ya mwisho kwa ajili ya kuongeza na kurekebisha vitu vichache vya kiufundi"

"Tumejipanga na tutahakikisha tunapata ushindi katika mechi yetu ya kwanza nyumbani," alisema Fadlu

Aidha Fadlu amebainisha kuwa anatambua mchezo hautakuwa mwepesi kwa sababu Bravos sio timu inayofungika kirahisi hivyo atahitaji kila mchezaji kujituma na kufuata mpango wa mchezo huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho

"Matatarajio yetu ni kupata alama tatu japo sio rahisi maana tunaujua ubora wa FC Bravos, tutatumia mbinu zetu ili kupata matokeo ya ushindi"

"Tunacheza na timu ngumu mechi yetu ya kwanza, tunahitaji nguvu ya mashabiki na nina imani Benjamin Mkapa itajaa," aliongeza Fadlu

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’