Manchester United wanafikiria kumuuza Joshua Zirkzee miezi sita tu baada ya kumsajili, huku Juventus ikimtaka mshambuliaji huyo wa Uholanzi, 23. (Corriere Dello Sport - In Italy)
Napoli wako tayari kumuuza Khvicha Kvaratskhelia msimu huu wa joto ikiwa mshambuliaji huyo wa Georgia hatasaini mkataba mpya, huku Manchester United wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sportmediaset – in Italy)
Mkufunzi mpya wa Mashetani Wekundu Ruben Amorim ametuma maskauti kumtazama winga wa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 wa Ureno Geovany Quenda mwenye umri wa miaka 26, mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres na winga wa Ureno Pedro Goncalves, 26, wakichezea Sporting dhidi ya Arsenal Jumanne. (Mail – Subscription Required)
Real Madrid wanataka kusajili beki mpya wa kulia na kumuona mlinzi wa Tottenham Pedro Porro mwenye umri wa miaka 25 kama shabaha inayowezekana. (Sport - Spanish)
Brighton wamemfanya mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, kupatikana kwa mkopo mwezi Januari. (Telegraph – Subscription Required)
Manchester United wanataka kusajili beki mpya wa kushoto msimu huu wa joto, huku beki wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 24 kutoka Canada Alphonso Davies na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa wa AC Milan Theo Hernandez, 27. (Sports in Spanish)
Brighton wamemfanya mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, kupatikana kwa mkopo mwezi Januari. (Telegraph - Subscription Required)
Manchester United wanataka kusajili beki mpya wa kushoto msimu huu wa joto, huku beki wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 24 kutoka Canada Alphonso Davies na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa wa AC Milan Theo Hernandez, 27, wakizingatiwa. (Florian Plettenberg)
Mholanzi Ruud van Nistelrooy, 48, ameivutia zaidi timu ya Leicester baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo. (Football Insider)
Arsenal wapo kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Ethan Nwaneri mwenye umri wa miaka 17 kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu. (Fabrizio Romano)
Manchester United wanatayarisha kandarasi ya kikazi kwa mshambuliaji Chido Obi-Martin wa Denmark atakapofikisha umri wa miaka 17 mwishoni mwa mwezi. (Tipsbladet - in Denish)
Chelsea wanatazamia kumsajili kiungo wa kati wa Watford na England walio chini ya umri wa miaka 16, Mathis Eboue, mtoto wa beki wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue. (Mail)
BBC



