Simba imeanza vyema kampeni ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos Fc ya Angola katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Jean Charles Ahoua ameendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu leo tena akifunga bao pekee la ushindi kupitia mkwaju wa mapema katika kipindi cha kwanza baada ya beki wa Bravos kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari
Simba ilitawala mchezo katika kipindi cha kwanza ikitengeneza nafasi kadhaa lakini umakini ulikosekana kwa washambuliaji Steven Mukwala, Kibu Denis na Ahoua wakishindwa kutumia nafasi hizo
Kipindi cha pili Bravos walirejea wakiwa imara na wangesawazisha bao hilo kama sio umahiri wa mlinda lango wa Simba Moussa Camara aliokoa mkwaju wa penati
Ni aina ya mechi ambayo mashabiki wa Simba watafurahia alama tatu lakini ni wazi kocha Fadlu Davids atahitaji kuendelea kukiboresha kikosi chake ili kuhakikisha malengo ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo yanafikiwa