Local,Normal News,Yanga, Namungo

Yanga yapania kuzindukia Ruangwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Nov 2024
Yanga yapania kuzindukia Ruangwa

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amewashukuru mashabiki waliosafiri kwa wingi kutoka jijini Dar es salaam na maeneo mengine kuelekea Ruangwa kuiunga mkono Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Ramovic amesema ni deni kubwa kwao kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo huo

Zaidi ya mabasi 10 yameondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea Ruangwa kuipa sapoti Yanga katika mchezo huo

"Kwakweli ni jambo la Kujivunia sana, Nawashukuru sana mashabiki wa Yanga wanaotoka Dar es Salaam leo usiku na Wanayanga Wote wanaokuja Kuisapoti timu yetu hapo kesho, mimi na Wachezaji wangu tunapaswa kuwalipa Furaha, Wameonesha Moyo na Mapenzi ya Dhati, tunajiandaa kuirejesha furaha yao," alisema Ramovic

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Ramovic amesema wako tayari na wanachohitaji ni kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu

"Tuna mchezo mgumu na muhimu sana hapo kesho, katika maandalizi yetu mpaka sasa kila kitu kipo vizuri, tunafahamu Namungo wana wachezaji wazoefu lakini sisi hatupo hapa kutafuta kingine zaidi ya alama tatu," alisema

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Denis Nkane amesema wanakwenda kwenye mechi hiyo huku wakifahamu deni walilonalo baada ya kupoteza mechi zilizopita

"Sisi kama Wachezaji tunatambua umuhimu wa alama tatu kwenye Ligi, tumekaa chini na kuzungumza wapi kwa Kuboresha, tunamsikiliza Mwalimu na kujituma kwa dhati ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, mchezo wa kesho ni mgumu lakini tupo kwaajili ya Kupambana na kushinda"

"Kwanza niwapongeze Wanayanga kwa mapenzi wanayoonesha, Nimesikia Leo wanasafiri kutoka maeneo mbalimbali na kuja kutusapoti, hili ni deni kwetu na tunapaswa Kulilipa, niwaombe Wanayanga wa Ruangwa nao waje kutusapoti kesho, tupo hapa kwa ajili ya kushinda," alisema

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’