International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili, Disemba 1 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili, Disemba 1 2024

Juventus wanafikiria kumnunua Liam Delap wa Ipswich na wametuma maskauti kumtazama mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia anazivutia Chelsea na Manchester United. (Mirror)

Klabu hiyo ya Italia pia inatazamia kumnunua mshambuliaji wa Manchester United kutoka Uholanzi Joshua Zirkzee, 23 kwa mkopo. (Gazzetta dello Sport)

Paris St-Germain wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea wa Ufaransa Christopher Nkunku mwenye umri wa miaka 27 na huenda wakamtoa mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, kwa kubadilishana naye. (TBR Football)

Winga wa Liverpool Federico Chiesa, 27, ni chaguo ambalo Napoli inafikiria kuchukua nafasi ya Khvicha Kvaratskhelia ikiwa mshambuliaji huyo wa Georgia hatatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A. (Il Napolista)

Aston Villa huenda wakamkumbuka Louie Barry kutoka kwa mkopo Stockport mwezi Januari na kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Championship, huku Sheffield Wednesday na Middlesbrough wakiongoza mbio za kumsaka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21. (Star)

Manchester United hawana uwezekano wa kumpa Christian Eriksen mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 32 ukikamilika mwishoni mwa msimu. (Florian Plettenberg)

Crystal Palace ni miongoni mwa vilabu vingi vya Ulaya vinavyohitaji kumnunua beki wa pembeni wa Lecce raia wa Denmark Patrick Dorgu. (CaughtOffside)

Manchester United imemruhusu mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, kuondoka kwa uhamisho. (Fichajes - kwa Kihispania) Everton hawana uwezekano wa kukamilisha mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Roma,Bryan Cristante, 29, wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 28, anaweza kuwa njiani kuondoka Real Madrid huku Real Betis wakiwa na nia ya kumrejesha mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal katika klabu hiyo. (Fichajes)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
4h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
9h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
14h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
14h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’