Azam Fc inaweza kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi leo kama itaibuka na ushindi dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Azam Fc wana alama 27 katika nafasi ya pili huku Simba inayoongoza ligi ikiwa na alama 28
Kama Azam Fc itashinda mchezo huo ugenini, itafikisha alama 31 na kuiondoa Simba kileleni
Mtanange huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 3 usiku. Kutakuwa na mechi nyingine mbili ambazo zitapigwa mapema leo
Pamba Jiji watakuwa wenyeji wa KenGold uwanja wa CCM Kirumba huku Coastal Union wakiikabiri Prisons huko Arusha




