International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 2 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 2 2024

Paris St-Germain wanajadiliana na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah kuhusu uhamisho wa bila malipo wakati mkataba wa mchezaji huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 32 utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Arsenal, Liverpool, Chelsea, na Tottenham wanamfuatilia mshambuliaji wa Borussia Dortmund wa timu ya taifa ya Uingereza ya chini ya miaka 21 Jamie Gittens. (Florian Plettenberg)

Manchester United, Tottenham, Barcelona na Paris St-Germain ziliwatuma wasaka vipaji wao kumfuatilia mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush mwenye umri wa miaka 25 akiichezea Eintracht Frankfurt katika Ligi ya Europa siku ya Alhamisi. (Mirror)

Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya Antoine Semenyo msimu huu, huku Liverpool wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji mshambuliaji huyo wa Ghana, 24. (Football Insider)

Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Roberto Olabe wa Real Sociedad ili kumrithi Edu kama mkurugenzi wa michezo wa Gunners. (Footmercato - kwa Kifaransa)

Bournemouth, Brentford na Southampton wanamtafuta mshambuliaji wa Ureno na klabu ya Wolves Fabio Silva, 22, ambaye yuko Las Palmas kwa mkopo. (Fichajes - kwa Kihispania)

Liverpool wanatumai kuwashinda Manchester United katika usajili wa Januari wa beki wa Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye Bournemouth ina thamani ya £40m. (CaughtOffside)

Newcastle wako tayari kumuuza beki wa zamani wa Uingereza Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 34 mwezi Januari. (Football Insider) Al-Hilal wako tayari kuchuana na Arsenal kwa ajili ya kumsajili winga wa Las Palmas mwenye umri wa miaka 21 wa Uhispania Alberto Moleiro. (Team Talk)

Luton ilazimika kulipa £1.5m kumfuta kazi kocha Rob Edwards kwa sababu ya mkataba wa miaka minne aliosaini msimu wa joto. (Sun)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’