Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane atakaa nje kwa muda kutokana na kupasuka kwa misuli ya paja, klabu hiyo imesema
Kane alitolewa nje baada ya dakika 33 katika sare ya 1-1 Jumamosi dhidi ya Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atakosa mechi ya 16 bora ya Kombe la Ujerumani la Bayern nyumbani dhidi ya mabingwa Bayer Leverkusen leo Jumanne
Bayern ilitoa taarifa siku ya Jumapili ikisema kuwa nahodha huyo wa Uingereza alipasuka msuli mdogo nyuma ya paja lake la kulia
Taarifa zaidi zimebainisha kuwa Kane huenda akakosa kucheza kwa wiki mbili
Bayern wamebakiza mechi tano zaidi mwaka 2024. Baada ya ziara ya Leverkusen, Bayern wanaikaribisha Heidenheim kabla ya kucheza na Shakhtar Donetsk mjini Gelsenkirchen, wakimenyana na Mainz kwenye Bundesliga na kuwakaribisha RB Leipzig katika mechi ya mwisho ya mwaka.