Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 06 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 06 2024

Arsenal na Chelsea zinamtafuta mshambuliaji na klabu hizo mbili za London zina orodha sawa ya wachezaji wanaowataka, ambayo ni pamoja na mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 25. (Caught Offside)

Manchester United pia imefanya usajili wa mshambuliaji kuwa kipaumbele chake katika uhamisho la Januari. (Mirror)

Bayern Munich wanajiandaa kumuongeza mkataba wa mchezaji wao wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies, huku Manchester United wakifahamu kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 24 huenda akasaini mkataba mpya licha ya kumtaka. (Floran Plettenberg, Sky Germany)

Manchester United wako nyuma ya Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Lecce raia wa Denmark Patrick Dorgu. (Team Talk)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter ameuliziwa na klabu za Wolves na West Ham. (Sportsport)

Kocha wa zamani wa Borussia Dourtmund Edin Terzic hatakuwa mkufunzi mpya wa West Ham ikiwa Lopetegui ataondolewa kwenye nafasi yake, lakini mkufunzi wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand yuko kwenye kinyang'anyiro. (Florian Plettenberg)

Kocha wa zamani wa West Ham David Moyes ni miongoni mwa wanaowania nafasi ya kazi katika klabu ya Wolves iwapo Gary O'Neil atafukuzwa (Telegraph - usajili unahitajika)

Liverpool wanawasiliana na Bayer Leverkusen kuhusu uhamisho wa beki wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23. (Caught Offside)

Manchester City itamruhusu kiungo wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 33, kujiunga na moja ya vilabu dada vya City Football Group atakapoondoka kwenye kikosi cha Ligi ya Primia. (Telegraph - usajili unahitajika)

Lakini Inter Miami ya David Beckham imemfanya De Bruyne kuwa shabaha yao kuu ya uhamisho. (Mirror)

Mshambuliaji wa Everton na Guinea-Bissau Beto, 26, na kiungo wa Mali Abdoulaye Doucoure, 31, wanasakwa na klabu ya Roma. (Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)

Liverpool wana uhakika mlinzi wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku mazungumzo yakiendelea kuhusu mkataba mpya. (Fabrizio Romano)

Juventus na Marseille wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Mfaransa Benoit Badiashile. (Caught Offside)

Chelsea imefanya mawasiliano na klabu ya Benfica kuhusu mpango wa kumsajili beki wa Ureno Tomas Araujo, 22, huku klabu hiyo ya London ikiwa tayari kumruhusu mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi, 26, kuondoka mwezi Januari. (Team Talk )

Mustakabali wa Fabio Vieira wa Arsenal katika klabu hiyo uko mashakani huku The Gunners wakiwa tayari kupokea ofa ya kumuuza kiungo huyo wa kati Mreno mwenye umri wa miaka 24, ambaye kwa sasa yuko Porto kwa mkopo. (Daily Mail - usajili unahitajika)

Mkurugenzi wa kandanda wa Barcelona Deco amekutana na wawakilishi wa beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28, ambaye mkataba wake katika klabu ya Bayer Leverkusen unamalizika msimu ujao. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
7h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
9h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
10h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
10h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
11h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
14h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
16h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
17h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
17h ago
READ MORE β†’