Simba imeacha alama zote tatu nchini Algeria baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya CS Constantine
Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' alifunga bao la Simba mapema dakika ya 20 akipiga krosi iliyojaa moja kwa moja kimiani
Hata hivyo dakika 5 za mwanzo kipindi cha pili zilikuwa majanga kwa Simba CS Constantine wakifunga mabao yao mawili dakika ya 47 Hamza akijifunga kabla ya Brahim kufunga la pili dakika ya 50
Kuingia kwa mabao hayo kuliifanya Simba izinduke na kupeleka mashambulizi langoni kwa CS Constantine lakini kukosekana umakini katika eneo la mwisho kulipelekea matokeo hayo kubaki hivyo kwa dakika zote 90
Mapema Bravos iliichapa CS Sfaxien na hivyo kuongeza ushindani katika kundi A
CS Constantine wanaongoza wakiwa na alama 6 huku Simba ikifuata nafasi ya pili ikiwa na alama 3 kama ilivyo kwa Bravos. Sfaxien wanaburuza mkia wakiwa hawana pointi
Disemba 15 Simba itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuikaribisha CS Sfaxien