Local,Normal News,Simba

Simba kumaliza hasira kwa CS Sfaxien

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Dec 2024
Simba kumaliza hasira kwa CS Sfaxien

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally amesema kuwa matokeo waliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwa walifanya makosa ndani ya dakika tano ambayo yaliwagharimu

Kwenye mchezo uliochezwa Desemba 8 2024 Simba walitangulia kufunga dakika ya 24 kupitia kwa Zimbwe na walifungwa mabao mawili kipindi cha pili dakika ya 47 kwa beki Hamza kujifunga na dakika ya 51 kupitia kwa nahodha wa CS Constantine, Jian

Ahmed amesema baada ya mchezo huo wanarejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya CS Sfaxien utakaopigwa Disemba 15 uwanja wa Benjamin Mkapa

"Matokeo tuliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya na kilichotokea hatuwezi kubadili sasa ni hesabu kuelekea mchezo wetu wa tarehe 15 ambapo tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wa hatua ya makundi"

"Kikubwa kuelekea kwenye mchezo wetu mashabiki tuungane kwenye kampeni za kusaka ushindi kwani matokeo yaliyopita tukiwa nyumbani tulipata pointi tatu na sasa ni kuelekea mchezo wetu wa pili tukiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa," alisema Ahmed

Mchezo unaofuata Simba inachuana na CS Sfaxine iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mbaoa 3-2 dhidi ya Bravos wote wakiwa kundi A ambalo vinara ni CS Constantine yenye pointi sita

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
58m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’