Kwa mara ya kwanza michuano ya kombe la Mapinduzi 2024/25 inatarajiwa kushirikisha timu za Taifa badala ya klabu kama ilivyofanyika miaka iliyopita
Michuano ya mwaka inatarajiwa kuanza Januari 03 na kumalizika Januari 10 2025 visiwani Zanzibar
Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars zitashiriki huku Kenya, Uganda, Burundi na Burkina Faso nazo zikithibisha ushiriki wao
Michuano hii itakuwa fursa timu za Taifa kujiandaa na michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika Tanzania, Kenya na Uganda mwezi February 2025
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha Tsh 100M



