Local,Normal News,Coastal

Matampi ataja sababu ya kuondoka Coastal Union

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Dec 2024
Matampi ataja sababu ya kuondoka Coastal Union

Aliyekuwa mlinda lango wa Coastal Union Vumiley Matampi amesema sababu iliyopelekea avunje mkataba wake na klabu hiyo ni madai ya malimbikizo ya mishahara

Matampi ambaye ndiye kipa bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita akimpindua Djigui Diarra wa Yanga aliyebeba tuzo hiyo misimu miwili mfululizo, amesema sio rahisi kwake kufanya kazi huku akiwa halipwi stahiki zake

Mkongomani huyo aliyejiunga na Coastal Union Agosti 2023, mkataba wake ulitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu baada ya msimu uliopita kutoa mchango wake mkubwa katika kuifanikisha timu hiyo kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Jana klabu ya Coastal Union ilitoa taarifa ya kuvunja mkataba wake na kumtakia kila la kheri katika safari yake ya soka

"Nilipewa barua wiki iliyopita na kwangu naona ni uamuzi mzuri tu ambao klabu imefikia kwani sikuwa napata haki yangu kama ilivyotakiwa. Sijalipwa mshahara wangu miezi mitatu, suala ambalo sio zuri kwa upande wangu, niko tayari sasa kwa changamoto mpya," alisema Matampi

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
58m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’