Baaada kukosa ushindi katika mechi nne zilizopita, Singida Black Stars leo imezinduka uwanja wa LITI ikiichapa Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Aliyekuwa mshambuliaji Mkenya Elvis Rupia aliyekuwa shujaa wa Singida BS siku ya leo akipachika mabao mawili katika kipindi cha kwanza ambacho Singida BS walitawala
Yassin Mgaza alifunga bao pekee la Dodoma Jiji katika kipindi cha pili ambacho vijana wa Meckie Mexime walirejea wakiwa imara zaidi
Rupia amefikisha mabao 7 na sasa ndiye kinara wa kuzifumania nyavu ligi kuu ya NBC msimu huu akimpiku Suleiman Mwalimu wa Fountain Gate mwenye mabao 6
Licha ya ushindi huo, Singida BS imesalia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikifikisha alama 27 sawa na Yanga ambao ina uwiano mzuri zaidi wa mabao