International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 13 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 13 2024

Mkufunzi wa United Ruben Amorim anasema ni wachezaji tisa katika kikosi chake ambao hawawezi kuuzwa, huku kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 30, na winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, wakiwa miongoni mwa majina yaliyo katika hatari ya kuuzwa. (Mail)

Klabu kadhaa kubwa za Ulaya zimeonyesha nia ya kumnunua beki wa pembeni wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 24 Alphonso Davies, ikiwemo Liverpool, Real Madrid na Barcelona. (Athletic - Subscription Required)

Manchester City wamekubali kuwa wanahitaji kununua wachezaji katika dirisha la usajili la Januari kufuatia mwenendo wao mbaya, huku kukiwa na uwezekano wa kusajili kati ya wanne hadi sita katika madirisha mawili yajayo. (Telegraph - Subscription Required)

City wanamtaka kiungo wa kati wa Valencia Muhispania Pepelu, 26, kutoa ulinzi kwa Rodri aliyejeruhiwa. (Estadio Deportivo)

Arsenal wako hatarini kumpoteza kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 31, bila malipo msimu wa joto. {Mirror)

Mshambulizi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 21 raia wa Uingereza Carney Chukwuemeka anavutia vilabu vya Ligi ya Premia. (Football Insider)

Mshambulizi wa Brazil Richarlison, 27, atakataa kutumwa kwa klabu ya zamani ya Fluminense anapojaribu kujithibitisha Tottenham. (TNT Sports Brazil - In Portuguese)

Manchester United wanamtaka mlinzi wa Girona Muhispania Miguel Gutierrez, 23, mwezi Januari huku wakionekana kuimarisha chaguo lao la beki wa kushoto. (TeamTalk)

Newcastle wanamfuatilia winga wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Maghnes Akliouche. Tottenham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ufaransa Andy Diouf, 21, baada ya kumtazama akiwa Lens. (GiveMeSport)

Spurs wanafikiria kumwita mlinzi wa Uingereza Ashley Phillips, 19, kutoka kwa mkataba wake wa mkopo huko Stoke mwezi Januari ili kusaidia kupunguza tatizo lao la majeraha. (Standard)

Wolves watalazimika kumuuza mmoja wa wachezaji wao nyota mwezi Januari ili kuepuka kuvunja sheria za Fifa (Football Insider)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Manchester United Dan Ashworth anaweza kuchukua nafasi ya Edu katika klabu ya Arsenal, hata hivyo Roberto Olabe wa Real Sociedad pia anazingatiwa. (Mail- Subscription Required)

Crystal Palace wanataka wachezaji watatu kutoka Lyon, huku winga wa Ghana Ernest Nuamah, 21, winga wa Ufaransa Rayan Cherki, 21, na mlinzi wa Ufaransa Sael Kumbedi, 19, wakiangaziwa. (TBR Football)

Mlinzi wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 30, anavutia vilabu kadhaa vya Serie A, ikiwemo AC Milan. (TeamTalk)

BBC

More Stories

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
3h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
5h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
9h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
9h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
10h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
22h ago
READ MORE β†’
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
1d ago
READ MORE β†’