Local,Normal News,Tabora, Azam

Tabora United, Azam Fc uso kwa uso ligi kuu leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Dec 2024
Tabora United, Azam Fc uso kwa uso ligi kuu leo

Tabora United na Azam FC zimetambiana kuelekea mchezo wa Ligi kuu bara utakaochezwa leo Desemba 13, 2024 kila mmoja ikijinasibu kufanya vizuri katika mchezo huo utaakopigwa Alsan Mwinyi mkoani Tabora.

Kocha wa Tabora United raia wa DR Congo Anicet Makiadi amesema kuelekea mchezo huo timu yake imejiandaa vyema licha ya changamoto lukuki ndani ya timu yake.

"Maandalizi yetu kueleeka mchezo dhidi ya Azam yako vizuri, tumekuwa na muda wa kupumzika baada ya mchezo wetu uliopita dhidi ya KMC lakini nathubutu kusema tuko tayari kwa mchezo, hapo nyuma tulipata matatizo kidogo ndani ya timu ambayo yaliathiri maandalizi yetu lakini hilo halituumizi kichwa kwani bado tunaendele ana mpango wetu wa kupata matokeo" amesema Makiadi

Aidha Makiad amesema mchezo dhidi ya Azam utakuwa mgumu kutokana na kiwango bora kinachoonyeshwa na Azam fc hasa baada ya ujio wa kocha mpya lakini anaamini nguvu wanayopewa na mashabiki wa timu hiyo itawasaidia kupata matokeo katika mchezo huo muhimu.

Nae Kocha mkuu wa Azam Rachid Taoussi amesema kuelekea mchezo dhidi ya Tabora atawaheshimu zaidi wapinzani wao kwakua ni timu kubwa.

"Kuelekea mchezo wetu na Tabora tunaamini utakuwa mchezo mgumu, tumeandaa mbinu zetu kuelekea huo mchezo lakini tunategemea ushindani mkubwa, kwanza uwanja utakuwa tofauti na ule tuliozoea lakini hilo halitatuzuia kupatambana kupata ili kufanikisha azma yetu"

"Nimezungumza na wachezaji tumejianda kisaikolojia kwenye huu mchezo kwani tunatakiwa kushinda kila mchezo kama mnavyoona Tabora imekuwa na kiwango bora kwenye michezo yake hivyo mpaka kufika hapa tumejiandaa na tunaitaka mechi" Taoussi amenukuliwa na Mwanaspoti

Mechi nyingine ambayo inatarajiwa kupigwa leo ni kati ya Fountain Gate dhidi ya Coastal Union ikipigwa uwanja wa Kwaraa, Manyara

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
4m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
3h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
5h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
9h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
10h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
22h ago
READ MORE β†’