Azam Fc jana iliendeleza dhamira yake ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu wakiichapa Fountain Gate mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Azam Complex
Ilikuwa siku nyingine ya kuzishuhudia 'shoo' za kiungo mahiri wa timu Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye jana aliongeza assist yake ya 7 msimu huu na kufikia rekodi aliyoweka msimu uliopita
Katika msimu wa 2023/24 Fei Toto alitumia mechi 30 kufunga mabao 19 na kutoa assist 7, mpaka sasa msimu huu amepachika mabao 3 na kutoa assist 7 ndani ya mechi 15 akiwa amehusika katika mabao 10
Kilichopungua msimu huu kutoka kwake ni idadi ya mabao ya kufunga na pengine hilo linatokana na mabadiliko ya benchi la ufundi ambayo yamepelekea kiungo huyo kupewa majukumu tofauti ya kuchezesha na kutengeneza nafasi zaidi



