Local,Normal News,Yanga, Mashujaa

Yanga, Mashujaa kumaliza ubishi KMC Complex leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Dec 2024
Yanga, Mashujaa kumaliza ubishi KMC Complex leo

Baada ya kutoka katika mashindano ya kimataifa, mabingwa watetezi, Yanga wanatarajia kuwakaribisha Mashujaa FC kutoka Kigoma katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam huku makocha wakitamba utakuwa mchezo wa ufundi zaidi

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, amesema ameiangalia vizuri Mashujaa na kubaini ni timu nzuri, hivyo anakwenda kuwakabili kwa tahadhari na watatumia mifumo tofauti katika mechi hiyo

Ramovic alisema anaweza kubadilisha mfumo kutokana na mchezo utakavyokuwa unaendelea kwa lengo la kuhakikisha wanapata matokeo chanya

"Najua tunatakiwa tuonyeshe sisi ni nani, kila timu tunaiheshimu na kila mechi tunakwenda kucheza kwa plani tofauti, tunahitaji kushinda na kukaa sehemu salama, kwa sababu mechi zimekuwa nyingi sasa za ligi kuu na timu zilizo juu zimekuwa zikipata ushindi"

"Kama hatuweka mkazo, kupambana kwenye mchezo huwezi kushinda, kama huwezi kukimbia uwanjani kama una mpira na kumkimbiza mpinzani wakati hauna mpira, basi huwezi kufanya kitu, tumemuangalia mpinzani wetu na tunajua jinsi gani tunakwenda kupamba naye kimbinu na kifundi," alisema Ramovic

Kocha huyo pia amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa wavumilivu kwa sababu bado ana muda mchache sana tangu alipojiunga na katika kikosi hicho

"Kama nilivyosema nimekuja hapa nina wiki tatu tu, sina 'pre season',nimekuta timu imepoteza wachezaji muhimu wanne kwa majeraha, haiwezi kuwa rahisi, lakini hakuna hata mmoja anayetaka kujua kuhusu hilo,wanachohitaji ni matokeo moja kwa moja, ukweli ni presha kubwa lakini kwangu ndicho kitu ambacho nimezoea kuishi, tupo hapa kufanya kazi ili tushinde mechi za Ligi Kuu, kuhusu Ligi ya Mabingwa si muda wake hivi sasa," alisema kocha huyo

Naye Kocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed 'Bares', alisema timu yake inazihitaji zaidi pointi tatu kwa 'udi na uvumba'

"Utakuwa ni mchezo mkubwa, kwetu sisi ni muhimu, tunajua tunacheza na timu kubwa, iliyosheheni wachezaji bora, lakini sisi upande wetu tumejiandaa vizuri zaidi ukilinganisha na michezo yote iliyopita, tunahitaji pointi tatu ili tufike kule tunakotarajia"

"Sina shaka utakuwa ni mchezo wa kimbinu zaidi na kiufundi, tunajua Yanga ni timu inayochezea sana mpira ina viungo wazuri, ila sisi ni timu ambayo tunabadilika kutokana na timu tunayocheza nayo kwa hiyo tunatakikisha tunawadhibiti katika maeneo hayo, mbinu nyingine si vyema sana kuisema hapa,"alisema.

IPP Media

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’