Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, KMC

Mwenyekiti Kamati ya uchaguzi Dar afungiwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Dec 2024
Mwenyekiti Kamati ya uchaguzi Dar afungiwa

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia miaka mitano kujihusisha na mpira wa miguu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salam (DRFA), Yusuph Kaiwanga

Katika uamuzi wake, Kamati imesema baada ya kupitia ushahidi wa nyaraka na maelezo ya shahidi imejiridhisha pasi na shaka kuwa Mlalamikiwa Kaiwanga alitenda makosa kwa makusudi

Kamati ilijiridhisha kuwa Mlalamikiwa hakutumia vyema mamlaka aliyopewa kisheria kusimamia uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke (TEFA) na kuamua kuufuta

Hatua yake ya kuufuta haikuwa sahihi kwa vile alishiriki mchakato mzima wa uchaguzi huo

Hivyo, Kamati ya Maadili imeamua matokeo ya uchaguzi wa TEFA yanabaki kama yalivyo

Mbali ya kifungo cha miaka mitano, Kamati pia imemtoza mlalamikiwa faini ya sh. milioni sita

Adhabu hizo zimetolewa chini ya kifungu cha 73(4) na (5) cha Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2021

Awali Kaiwanga alilalamikiwa mbele Kamati ya Maadili kuwa kitendo chake cha kufuta Uchaguzi wa TEFA wakati alishiriki mchakato mzima tangu mwanzo kilikiuka Kanuni za Maadili za TFF.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’