International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 20 2024

Joel JJ By Joel JJ
20 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 20 2024

Manchester United inamchunguza Ederson wa Atalanta, 25, na kiungo huyo wa kati wa Brazil ni mmoja wa wachezaji wachache ambao klabu hiyo inazingatia sana kusaini kwa nafasi hiyo. (Florian Plettenberg)

West Ham, Leicester City na Southampton wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20 kutoka Brighton. (Givemesport)

Southampton wanaweza kumuuza mchezaji wao chipukizi Tyler Dibling, 18, ikiwa watashuka daraja kutoka Ligi ya Premia, huku Manchester United na Newcastle zikiwa na nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uingereza. (Football Insider)

Uvumi kwamba kiungo wa zamani wa Manchester United na Juventus Paul Pogba, 31, alikuwa ameonekana kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester City haukuwa wa kweli. (Fabrizio Romano)

West Ham, Fulham, na Crystal Palace wote wanamfuatilia kiungo wa Juventus Nicolo Fagioli, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 23 ameivutia Tottenham hapo awali na huenda akapendelea kujiunga na klabu hiyo. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Chelsea wanafikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21. (TeamTalks)

Hapo awali Arsenal walifanya mazungumzo kuhusu kutaka kumnunua Sesko na kubaki na nia ya kumnunua mchezaji huyo ambaye ameanzisha uhusiano mzuri na wawakilishi wake. (Mail Plus - Subscription Required)

Bosi wa West Brom Carlos Corberan na meneja wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand ni miongoni mwa wagombea kuchukua nafasi ya Russell Martin huko Southampton, lakini bosi wa muda Simon Rusk atasalia kuinoa kwa safari ya Jumapili ya Fulham. (Sky Sports)

Klabu ya Saudi Pro League, Al-Shabab inavutiwa na dili la bei iliyopunguzwa kwa mlinda lango wa Newcastle Slovakia Martin Dubravka, 35. (I)

Wolves wanaweza kulenga uhamisho wa Januari kwa mlinzi wa kati wa Austria Kevin Danso, 26, ambaye Lens inaweza kutaka kumuuza. (L'Equipe - in French)

Kiungo mshambuliaji wa Monaco Mfaransa Maghnes Akliouche, 22, alisema angependa kuichezea Barcelona katika maisha yake ya soka. (Sport - In Spanish)

Winga wa Arsenal Reiss Nelson - ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Fulham - ataruhusiwa kuondoka The Gunners msimu ujao kwa kuwa kuna uwezekano mchezaji huyo wa miaka 25 hatokuwa sehemu kubwa ya mipango ya Mikel Arteta katika siku zijazo. (Mail Plus - Subscription Required)

Bosi wa zamani wa Coventry Mark Robins amekataa fursa ya kuzungumza na klabu nyingine ya Championship Millwall kuhusu nafasi yao ya umeneja. (South London Press)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
15h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
16h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
18h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
18h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
19h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
19h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
19h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
20h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
20h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
22h ago
READ MORE →