International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Disemba 22 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Disemba 22 2024

Napoli wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Manchester United na England Harry Maguire, huku Galatasaray pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 Old Trafford. (Athletic - subscription required)

Mshambulizi wa Paris St-Germain Randal Kolo Muani, 26, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo ya Ligi 1 mnamo mwezi Januari, huku klabu kadhaa za Ligi ya Primia zikimhitaji Mfaransa huyo (Florian Plettenberg)

Mshambulizi wa Chelsea Christopher Nkunku, 27, yuko tayari kuondoka mwezi Januari baada ya kukosa muda wa kucheza, huku Paris St-Germain, Fenerbahce na Galatasaray zote zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (TBR Football)

Tottenham wanapanga kuweka dau la pauni milioni 20 kumnunua mlinda mlango wa Burnley wa England chini ya umri wa miaka 21 James Trafford, ambaye atakuwa na umri wa miaka 22, mwezi ujao. (Mirror)

Manchester United wako tayari kushindana na Arsenal katika juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 . (Football Insider)

Barcelona, Tottenham, Manchester United na Chelsea wote wanavutiwa na winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 28. (Sport - in Spanish)

Kipa wa zamani wa Ujerumani Manuel Neuer, 38, huenda akasaini mkataba mpya wa kusalia Bayern Munich hadi 2026. (Florian Plettenberg)

Ipswich Town na West Ham United wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Galatasaray na Morocco Hakim Ziyech, 31, kwenye Ligi ya Primia. (Fichajes)

Tottenham wanamwinda winga wa Borussia Dortmund na Ujerumani Julian Brandt, 28. (Football Transfers) Arsenal wanasalia kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting CP na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, ingawa mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko ndiye wanayemlenga zaidi kwa sasa. (Football)

Crystal Palace wanajitahidi kufikia makubaliano ya kumsajili winga wa Ujerumani Jan-Niklas Beste, 25, kutoka Benfica. (Sacha Tavolieri)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’