International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 23 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 23 2024

Mpango wa Liverpool kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro huenda ukalazimika kusubiri hadi msimu wa joto kwani matakwa ya Seagulls kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yatafanya uhamisho wa Januari kuwa mgumu. (Football Insider)

Paris St-Germain wako tayari kulipa euro 100m (£83m) kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Fichajes.net – in Spanish)

PSG ya Ufaransa pia inatazamia kulipa euro 58m (£48m) kama kifungu cha kutolewa cha Athletic Bilbao kwa winga wa Uhispania Nico Williams - lakini Manchester United na Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (El Desmarque – In Spanish)

Barcelona wamepoteza imani na kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong na inaonekana kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka katika klabu hiyo ya Uhispania. (Relevo – In Spnish)

Leicester City wanapanga mpango wa pauni milioni 8 kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Valentin Gomez, 21, kutoka Velez Sarsfield. (Sun)

Newcastle ni moja ya klabu zinazomtaka beki wa Barcelona Eric Garcia, 23, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City anataka kusalia Nou Camp na kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza. (Sport – In Spanish)

Crystal Palace wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Benfica Mjerumani Jan-Niklas Beste, 25, mwezi Januari. (Sky Sports Switzerland)

Real Madrid wanamfikiria beki wa kati wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Rafa Marin, 22, ambaye alifanya mazoezi katika akademi yao ya vijana na kwa sasa anachezea Napoli. (Fichajes.net – in Spanish)

Blackburn Rovers na Burnley wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Sheffield United kutoka Scotland Oli McBurnie, 28, kutoka Las Palmas ya Uhispania. (Sun)

Winga wa Uhispania Lamine Yamal, 17, anakaribia kuongeza mkataba wake na Barcelona hadi 2030. (Nicolo Schira)

Newcastle itamruhusu mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 32, kuondoka bila malipo kandarasi yake itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’