International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Disemba 25 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Disemba 25 2024

Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen mwezi Januari, huku Napoli wakiwa tayari kwa mkataba wa kubadilishana wachezaji kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray. (TBR Football)

Everton wanajiandaa kumpa kipa wa England Jordan Pickford, 30, mkataba mpya ambao utamweka katika klabu hiyo kwa maisha yake yote yaliyosalia. (TBR Football)

Chelsea, Arsenal na Tottenham zote zimetuma maskauti kumtazama beki wa pembeni wa Club Brugge na Ubelgiji Maxim de Cuyper, 24. (Caughtoffside)

FC Zurich wamewasiliana na Arsenal kuuliza kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Uingereza Nathan Butler-Oyedeji, 21, mwezi Januari. (Football Insider)

Paris St-Germain huenda wakaipa Arsenal nafasi ya kumsajili fowadi wao wa nje wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26. (Standard)

Bosi wa Brighton Under-18s Inigo Calderon, 42, yuko kwenye mazungumzo ya juu ili kuwa meneja mpya wa Bristol Rovers. (Sky Sports)

Bayern Munich ina matumaini ya kutaka kumnunua kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21, ambaye yuko kwenye majadiliano na Bayer Leverkusen kuhusu mkataba mpya. (Sky Germany)

Mkufunzi wa Leicester City Ruud van Nistelrooy anaweza kuegemea kwenye uhusiano wake na Manchester United ili kupata saini ya mkopo inayofaa Januari. (Football Insider)

Manchester United walianza kutafuta mrithi wa muda mrefu wa Erik ten Hag mara tu meneja wao wa zamani Mholanzi alipotia saini mkataba mpya msimu wa joto. (Telegraph – Subscription Required)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’