International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 27 2024

Joel JJ By Joel JJ
27 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Disemba 27 2024

Manchester United wameweka bei ya takriban £50m kumuuza mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 27. (Caughtoffside)

Liverpool wana uhakika mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, ambaye mkataba wake unamalizika majira ya joto, atasaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo. (Team Talks)

Real Madrid hawana nia ya kumsajili Van Dijk msimu huu wa joto, licha ya ripoti kuwahusisha na Mholanzi huyo. (Marca - In Spanish)

Beki wa kushoto wa Bayern Munich Alphonso Davies, 24, yuko tayari kuhama Ligi ya Premia msimu huu, huku Manchester United na Liverpool zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji Mkanada huyo. (TBR Football)

Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa Wolves Mbrazil Matheus Cunha, 25, ambaye anaweza kupatikana ikiwa klabu hiyo ya Midlands itashushwa daraja kwenye Ubingwa. (Athletic - Subscription Required)

Winga wa Brazil Antony amekuwa na ofa za kuondoka Manchester United mwezi Januari lakini klabu hiyo haitaki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aondoke, kulingana na wakala wake. (Give Me Sport)

Wakala wa Dani Olmo amewasili Manchester huku klabu za Ligi ya Premia, zikiwemo Manchester United na Manchester City, zikitaka kuchukua fursa ya matatizo ya Barcelona kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uhispania, 26, kabla ya tarehe ya mwisho ya Januari 1. (Mail)

Kuna "nafasi kubwa" ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, ambaye amevutia Manchester United na Liverpool, kuhamia Ligi ya Premia Januari. (Football Transfers)

Fiorentina wanavutiwa na beki wa pembeni wa Parma mwenye umri wa miaka 25 Woyo Coulibaly. (Matteo Moretto - In Italy)

Kocha wa kikosi cha kwanza cha Liverpool John Heitinga anaongoza orodha ya watu wanaowania kuchukua nafasi ya Carlos Corberan kama kocha wa West Brom. (Football Insider)

Sporting Lisbon wanatazamiwa kujaza nafasi ya Joao Pereira, ambaye alitimuliwa siku ya Krismasi, na kocha wa Vitoria Guimaraes, Rui Borges. (Sky Sports)

BBC

More Stories

APR FC knock Aigles du Congo out of the CAF Champions League
APR FC knock Aigles du Congo out of the CAF Champions League
16m ago
READ MORE →
Azam FC Mourns U-20 Goalkeeper Iddy Salim After Motorcycle Accident
Azam FC Mourns U-20 Goalkeeper Iddy Salim After Motorcycle Accident
3h ago
READ MORE →
Gaborone United Coach Connor Confident Ahead of Yanga Decider
Gaborone United Coach Connor Confident Ahead of Yanga Decider
5h ago
READ MORE →
Mngqithi Warns Yanga Against Complacency Ahead of Gaborone United Decider
Mngqithi Warns Yanga Against Complacency Ahead of Gaborone United Decider
7h ago
READ MORE →
Official: João Pedro wins Premier League Player of the Month award for August
Official: João Pedro wins Premier League Player of the Month award for August
9h ago
READ MORE →
Simba targets CAF Champions League group stage, with semi-finals as the bigger ambition
Simba targets CAF Champions League group stage, with semi-finals as the bigger ambition
10h ago
READ MORE →
NBC Premier League: Libasse Gueye beats Mwajanga and Nzengeli to Player of the Month award
NBC Premier League: Libasse Gueye beats Mwajanga and Nzengeli to Player of the Month award
10h ago
READ MORE →
Fei Toto Keeps Quiet on Simba and Yanga Links as Azam Remains His Focus
Fei Toto Keeps Quiet on Simba and Yanga Links as Azam Remains His Focus
12h ago
READ MORE →
Expert Predictions for 21 Matches Taking Place Today, September 11, 2026
Expert Predictions for 21 Matches Taking Place Today, September 11, 2026
15h ago
READ MORE →
UEFA Champions League: results from tonight
UEFA Champions League: results from tonight
23h ago
READ MORE →