Local,Normal News,Yanga, Fountain

Yanga yaibamiza Fountain Gate 5-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Dec 2024
Yanga yaibamiza Fountain Gate 5-0

Yanga imerejesha 5G katika ligi kuu ya NBC leo wakiichabanga Fountain Gate mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex

Yanga ilitawala mchezo huo tangu mwanzo wa kipindi cha kwanza lilikuwa ni suala la muda kwa Yanga kuanza kuhesabu mabao kutokana na mashambulizi mfululizo waliyopeleka langoni kwa Fountain Gate

Alikuwa ni Pacome Zouzoua aliyefunga kalamu ya mabao akiunganisha krosi ya Chadrack Boka kutoka upande wa kushoto

Yanga ikaongeza mabao mengine mawili kabla ya mapumziko kupitia kwa Mudathir Yahya na Pacome kwa mara nyingine

Pacome almanusra aondoke na hat-trik shuti lake la mapema kipindi cha pili likiguswa na mlinda lango wa Fountain Gate John Noble kabla Shiga kumalizia mpira uliogonga mwamba

Clement Mzize ndiye aliyekamilisha kipigo kwa Fountain Gate akimalizia mpira kutoka kwa Salum Abubakar 'Sure Boy'

Ni ushindi wa tano mfululizo kwa kocha Sead Ramovic Yanga ikikusanya alama 15 chini yake na kufunga mabao 18

Yanga sasa ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi msimu huu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’