Al Hilal wamekufa sebuleni kwao Yanga ikichukua alama tatu muhimu katika mchezo wa raundi ya tano ligi ya mabingwa barani Afrika
Shuti la nje ya 18 kutoka kwa Stephane Aziz Ki lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu ambao sasa unaweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali
Yanga sasa inahitaji ushindi wa aina yoyote nyumbani dhidi ya MC Alger ili kutinga robo fainali
Haikuwa mechi nyepesi lakini wachezaji wa Yanga wameonyesha kwa vitendo kuwa wanaitaka robo fainali
Dakika 90 za mechi ya kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya MC Alger Januari 18 zitakamilisha mpango wa Yanga kufuzu robo fainali
INAWEZEKANA....!