International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, January 13 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Jan 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, January 13 2025

Mlinzi wa kulia wa Uingereza Kyle Walker, 34, anatazamiwa kusaini kandarasi ya miaka miwili na nusu na AC Milan na kufanikiwa kuhama kutoka Manchester City siku zijazo (Telegraph)

Walker anaweza kujiunga na wapinzani wa Milan Inter Milan kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail) Timu kutoka Saudi Pro League zimesalia na nia ya kumsajili Walker, lakini beki huyo anataka kusalia Ulaya. (Sky Sports)

Meneja wa Napoli Antonio Conte anamtaka winga wa Manchester United Alejandro Garnacho, 20, kuchukua nafasi ya winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, ambaye anatarajiwa kuhamia Paris St-Germain. (Sport Italia)

Beki wa Uruguay Ronald Araujo, ambaye amekuwa akihusishwa na Juventus, anataka kuondoka Barcelona haraka iwezekanavyo, lakini klabu hiyo ya Catalan ina nia ya kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mundo Deportivo)

Beki wa Ujerumani Mats Hummels, 36, hana haraka ya kuanza mazungumzo juu ya kuongezwa kwa mkataba katika klabu ya Roma, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwezi Juni. (Soka Italia)

West Ham wako tayari kuleta mshambuliaji mpya baada ya kujua ukubwa wa jeraha la msuli wa mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, alilopata katika mechi ya Ijumaa ya Kombe la FA dhidi ya Aston Villa. (Fabrizio Romano)

Monaco wamewasilisha ombi la kumnunua kiungo wa West Ham Edson Alvarez, 27, baada ya ofa ya kumchukua kwa mkopo mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico kukataliwa na The Hammers. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Brighton ya Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, na mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27, wamehusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda West Ham. (TBR Football)

Atalanta wanataka kukamilisha usajili wa Januari wa mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kuelekea Newcastle United msimu wa joto kwa uhamisho wa bure. (Sun)

Bayern Munich wamempa mlinzi wa Canada Alphonso Davies, 24, mkataba mpya wenye thamani ya euro 25m (£21m) huku Real Madrid wakipania kumsajili kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto. (Marca)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’